Tunachoamini

Kutoka Oil4All
Rukia: urambazaji, tafuta

OpenOil iliundwa kwa imani kwamba uundaji wa sera wenye maendeleo ya kiubunifu, kiutendaji na kijamii katika shughuli za mafuta na gesi ni muhimu kwa maisha yetu ya baadaye kiujumla, na unawezekana ndani ya vikwazo vilivyopo sasa hivi.

Ni kweli kwamba kuelemea kwetu kunakoendelea kwenye matumizi ya haidrokaboni ni suala baya. Na ni kweli kwamba tunahitaji kuweka msisitizo zaidi kwa vitu vinavyoweza kutengenezwa upya. Lakini hata kwa upanuzi mkubwa wa nishati mbadala zinazoweza kufikiriwa, hakuna mwenye mpango wa kuaminika kuhusu uchumi unaoepuka kaboni kabla ya mwaka 2030. Hadi hapo, shughuli za mafuta na gesi zitaendelea kuchukua nafasi kubwa katika mafanikio na maendeleo ya dunia – au kinyume chake. Kukataa kuendana na ukweli huo ni hatari na ni kutokuwajibika.

Laana ya Rasilimali inaendelea kuathiri maisha ya mamilioni ya watu. OpenOil inaamini kwamba uzalishaji wa mafuta na gesi unaweza kuwafaidisha wananchi wa nchi zinazozalisha rasilimali hii kwa ufanisi zaidi, na madhara yaliyosababishwa na serikali zenye usiri na zisizo na demokrasia, mara zote kutokana na faida inayopatikana kwa kudhibiti utajiri wa rasilimali asilia, yanaweza kupunguzwa na kubadilishwa.

Kukosekana kwa uhakika kunakoendelea kuhusu mafuta kiasi gani yamesalia, na kwa gharama gani yanaweza kupatikana, pia kunafanya usalama wa nishati ya dunia kuwa ni suala la kuangaliwa kwa makini. Diplomasia ya rasilimali inakuwa na uzingativu zaidi wakati mizozo mipya ya rasilimali ikiwa inaonyesha dalili ya kuibuka. Tunahitaji njia bora zaidi kuhakikisha ugavi wa nishati uliothabiti zaidi na fikra za muda mrefu kuhusu hitajio la nishati.

OpenOil inaamini kanuni za kiujumla zifuatazo:

• Haja moja kubwa ni ya kufikiria kwa ubunifu zaidi. Hali ya udunifu wa uundaji wa sera katika shughuli za uchimbaji mafuta na gesi inatisha mno, pamoja na ukweli kwamba ni muhimu na inapata huu mzingatio mkubwa duniani. OpenOil inalenga katika kuendeleza mijadala mipana na ya kina duniani kote, na matokeo yanayoweza kutendewa kazi. Kulaani na kutiana ubaya kwa kificho havijawahi kuleta sera nzuri au matokeo mazuri.

• Jitihada za sasa hivi kuhusu uwazi na utawala ni lazima, lakini hazitoshelezi. Mkakati wa Uwazi katika Shughuli za Uchimbaji Rasilimali (Extractive Industries Transparency Initiative - EITI) umefanikiwa kuufanya uwazi kuwa sehemu ya utaratibu, kwamba kampuni na serikali zimeingia katika msukumo wa kukubaliana nalo. Lakini EITI inashughulikia upande mmoja wa uwazi katika mlolongo wa thamani, na kwa namna yoyote haiangalii ni uwazi kiasi gani, kama unavyotafsiriwa sasa hivi, unaweza kuleta maboresho na mabadiliko ya sera. Uwazi kiukweli ni sera endelevu ambayo imefanikisha mvuto katika shughuli ya mafuta leo hii na ni lazima uheshimiwe kwa hilo. Wakati huohuo, ni lazima tuende mbele zaidi ya hapo.

• Ubunifu wa sera lazima uwekwe kwenye msingi wa uhalisia wa masuluhisho yasukumwayo na soko. Mafuta ni shughuli ya ushindani kwa ajili ya faida na yataendelea kuwa hivyo. Jitihada za mwanzo kutaka kupunguza tamaa ya kodi na mabadiliko ya ghafla lazima ziendane na zisipingane na mienendo ya soko, kwa kujaribu kupunguza hatari kwa wahusika wote, kwa kuzungumzia tatizo la wakati huu la kutokuwa na mfumo mmoja, kwa mfano, au kwa kazi ya kijiolojia iliyotolewa fedha na serikali.

• Malipo ya faida ya mafuta moja kwa moja kwa raia kama inavyofanyika katika jimbo la Alaska nchini Marekani, ni wazo la kisera linalohitaji uangalizi mpana na nafasi ya utekelezaji katika ngazi ya nchi. Yakipangwa kwa njia tofauti, malipo ya moja kwa moja yanaweza yakawatoa makumi ya mamilioni ya watu kwenye umaskini na yakachangia kwenye Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) na vile vile kujenga uhusiano tofauti kabisa kati ya wananchi wa nchi zizalishazo mafuta na serikali zao.

• Ruzuku kwenye sekta ya mafuta mara zote imekuwa ni wazo baya ambalo linawafaidisha matajiri zaidi kuliko masikini na zinatia nguvu ufisadi. Jukumu la dola kwa raia wenye mahitaji lapaswa kutekelezwa kwa njia nyinginezo.

• Sekta binafsi kwenye nchi zenye utajiri wa mafuta zinaweza na zinapaswa kushirikishwa kimfumo kwenye suala la uwazi na haki za wanahisa kama zinavyohusika moja kwa moja na uongozi husika katika shughuli za mafuta. Sambamba na suala hili ni uhuru wa kupata habari.

• Mijadala mitatu ya kidunia inafanyika sasa na ambayo inahitaji kuunganishwa: Mabadiliko ya Hali ya Hewa, Uhaba na Usalama wa Nishati, na Laana ya Rasiliamali. Inatubidi tujitahidi zaidi na kutengeneza sera ambazo zinaelezea masuala mawili kati ya hayo au yote matatu kwa wakati mmoja, badala ya kutenganisha kila suala na kutoa ajenda za sera ambazo, kwa kutoziunganisha, zinakuwa hazitekelezeki. OpenOil inalenga kuwa kwenye kiini cha fikra zilizounganishwa.

• Vyombo vya habari ni sehemu muhimu ya utambuzi na ambayo inapuuzwa katika shughuli za uchimbaji wa mafuta. Mipango ya muda mrefu inahitajika kujenga uwezo na umahiri katika masuala ya nishati miongoni mwa waandishi wa habari. Katika nchi zinazotegemea mafuta kama chanzo kikuu cha mapato, kujenga utaalamu kunapaswa kuanzia na mafuta kwa sababu ya jukumu lake kuu katika uchumi, na kisha baadaye kushughulikia aina nyingine za nishati.

• Matumizi ya mitandao ya kijamii na vyanzo huru vya habari vina mchango mkubwa katika kutengeneza mazingira ya uwazi katika shughuli ya uchimbaji wa mafuta.